Bungeni:
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda amesema kuwa wizara yake imetekeleza vipaumbele vitano muhimu vilivyolenga kuboresha ubora wa elimu, kupanua fursa za kujifunza na kuimarisha matumizi ya sayansi na teknolojia nchini.
Amesema vipaumbele hivyo ni: Utekelezaji wa sera, mitaala na mapitio ya sheria pamoja na uandaaji wa miongozo ya utoaji elimu.
Kuongeza fursa na kuimarisha mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi.
Kuimarisha ubora wa elimu ya awali, msingi, sekondari na mafunzo ya ualimu.
Kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu.
Kuimarisha uwezo wa nchi katika utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara bungeni kwa mwaka wa Fedha 2026/2027 Waziri Mkenda amesema utekelezaji wa vipaumbele hivyo umeendelea kuleta matokeo chanya katika kuongeza ujuzi, kukuza ubunifu na kuandaa rasilimali watu yenye ushindani kwa mahitaji ya sasa ya soko la ajira.
